DAWA ZA KULEVYA ZATAWALA BUNGENI DODOMA


Bunge limeanza leo mjini Dodoma na sasa ni kipindi cha maswali na majibu ambapo hoja inayoendelea kwa sasa ni wabunge kutaka wahusika wa biashara ya dawa za kulevya watajwe.

Waziri Lukuvi ameahidi kuwataja na ametaka mwenye ushahidi apeleke.Hata hivyo, wabunge wamemzomea na spika ameonya hiyo tabia ya kuzomea.

Baadhi ya wabunge waliotaka majina yatajwe ni mh.Mama Kilango wa CCM na mbunge wa karatu kupitia CHADEMA ambae amehoji inakuwaje hata Raisi amekiri kuwa na orodha ya wauza unga bila wahusika kutajwa na kuchukuliwa hatua.


Hata hivyo,waziri Lukuvi amesisitiza umuhimu wa kuwa na ushahidi kwani amesema kama ni kutajwa tu na wengine wamo humu bungeni na ameongeza hata gazeti la Jambo leo limewataja kwahiyo kitu muhimu ni ushahidi na sio kutaja tu.


Vile vile mh.Lukuvi ameeleza nia ya serikali kubadilisha sheria ili madawa ya kulevya yakishakamatwa na ushahidi kupatikana(kuwa kwenye kumbukumbu) basi madawa hayo yaharibiwe mara moja kuliko utaratibu wa sasa ambao madawa hayo huhifadhiwa mpaka kesi husika kuisha na ametoa mfano wa madawa kuwekwa kwa miaka hata kumi kusubiri kesi ikamilike.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo