
Na Juma Mtanda, Morogoro.
JUMLA
ya kunguru weusi 482,183 wameuawa katika kipindi cha miaka mitatu
katika mikoa minee tangu kuanza kwa mpango wa kudhibiti kunguru weusi na
panya Tanzania ulioanza mwaka julai 2010 hadi januari 2012.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi mjini Morogoro Mtaalam wa kudhibiti kunguru
weusi na panya Tanzania, Adili Ngujiy alisema kuwa jumla ya kunguru
weusi 482,183 tangu kuanza kwa mpango wa kuwadhibiti.
Ngujiy
alisema kuwa kunguru hao wameuawa katika vipindi tofauti kati ya julai
mwaka 2010 na januari 2012 kwa njia mbili tofauti za kuwekewa sumu na
mitengo ambapo kat
ika jiji la Dar es Salaam limefanikiwa kuuawa kunguru 22,894 huku jiji la Tanga likiua kunguru 3216 wakati Kibaha likiwaua 1268.
“Tangu
kuanza kwa mradi wa kuua kunguru Tanzania ulianza mwaka 1996 kuwatega
kwa mitego pekee kwa jiji la Dar es Salaam na mwaka 2006 iliongezwa
mbinu ya kuwaua kwa kutumia sumu katika programu iliyokuwa ikiendeshwa
na wizara ya maliasi na utalii pekee” alisema Ngujiy.
Aliongeza
Ngujiy kwa kusema kuwa baada ya kupata mafanikio programu ya kuua
kunguru hao iliongezwa mikoa mingine mingine mitatu ikiwemo Morogoro,
Pwani na Tanga baada ya kupata ufadhili wa mashirika ya Danida, Finida
na USA chini ya wizara ya maliasili na utali.
Alitaja
idadi ya mitego ya kuua kunguru hao katika mikoa hiyo kuwa Dar es
Salaam pekee ina mitego 450, Tanga 20 na Kibaha 12 ambapo jumla ya
kunguru imeua 27,378.
Kunguru
waliouawa kwa njia ya kuwekewa sumu ni 464,181 ambapo Dar es Salaam
imeua kunguru 306,772, Tanga 54,668, Pwani 15,078 na Morogoro 87,663
katika kipindi cha kuanzia julai 2010 mpaka februari 2012.
Ngujiy
alisema kunguru 22,894 wenyewe waliuawa kutumia mitego 482 iliyotegwa
katika miji ya Kihaba, Tanga huku Dar es Saalaam ikiwakilishwa na
Temeke, Kinondoni na Ilala.
Kunguru
hao wanadaiwa kuletwa na serikali ya uingireza kwa ajili ya kusafisha
mji Mkongwe mwaka 1890 ambao kazi kubwa ni kula uchafu na kuingia
Tanganyika wakati huo kuingia mwaka 1850 wakining’inia kwenye meli na
maboti.