BASI LA HOOD LAPATA AJALI NA KUUA MKOANI MBEYA






MNAMO TAREHE 04.08.2013  MAJIRA YA SAA 06:45HRS HUKO MSWISWI WILAYA YA MBARALI BARABARA YA MBEYA/IRINGA, GARI NO T. 159 AXM AINA YA SCANIA BUS MALI YA KAMPUNI YA   HOOD LIKIENDESHWA NA DEREVA OMARY  SAID, MIAKA 50, MZIGUA, MKAZI WA MABIBO DSM LILIGONGANA NA GARI NO IT.3014 TOYOTA COROLLA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA DEVIS  ANAMUNDE, MIAKA 28, MZAMBIA MKAZI WA MUNZE LUSAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA DEREVA HUYO PAPO HAPO.

 MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA MAGARI YOTE MAWILI NA DEREVA WA HOOD BUS AMEKAMATWA TARATIBU ZINAFANYWA ILI AFIKISHWE MAHAKAMANI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHANA MSAIDIZI WA POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.

NA MBEYA YETU BLOG


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo