WAKAZI wa kijiji cha Rukuma katika eneo bunge la Lari Kenya, Alhamisi hii walifurika nyumbani kwa mvulana mmoja wa umri wa miaka 17 aliyedaiwa kuwanajisi kuku wawili wa nyanyake kabla ya kuwaua na baadaye kujiua kwa kukunywa sumu.
Wakazi
walioshtushwa na kisa hicho walidai mvulana huyo alijiua kwa kunywa sumu
kwani kulipatikana chupa ambayo haikuwa na kitu ndani kwenye sakafu ya
nyumba yake.
Kulingana na
Paul Njenga, kijana huyo alipatikana akiwa amelala kitandani akiwa
amefariki huku mizoga ya kuku hao ikiwa kwenye sakafu, suala
lililopelekea wakazi kushuku aliwanajisi kwa zamu.
Watoto
waliokaribia nyumba hiyo ya chumba kimoja cha mvulana huyo, walifukuzwa
na wakazi ili waache kuchungulia maiti ya mvulana huyo na mizoga ya kuku
hao.
Bw Njenga alisema waliwaita maafisa wa polisi wa kituo cha Lari waliowasili baada ya muda mfupi na wakaanza uchunguzi wao.
“Mvulana huyu
aliwakamata kuku hao wa nyanyake na kuwafungia katika nyumba yake
ambako amekuwa akiwachafua. Aliposikia wanatafutwa, aliwaua na akanywa
sumu na akafariki,” alisema Bw Njenga.
Kamanda wa
polisi wa eneo hilo Bw Joshua Opiyo hata hivyo alipuuzilia mbali madai
kwamba mvulana huyo aliyemtaja kama Samuel Muranja aliwachafuakuku hao
kabla ya kufariki.
Bw Opiyo
alisema mvulana huyo ambaye alikuwa mwanafunzi wa shule ya upili ya
Kirenga alikuwa amekataa shule kwa muda wa miezi miwili kwa sababu
ambazo hazikuelezwa na familia.
Alisema
aliondoka nyumbani mnamo Agosti 6 na alipatikana Alhamisi asubuhi akiwa
katika nyumba yake iliyo kando ya nyanya yake ambaye huwa wanaishi naye
akiwa amefariki.
Uchunguzi
Hata hivyo,
licha ya Bw Opiyo kupuuzilia mbali habari hizo, alisema mwili wa mvulana
huyo ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha City jijini
Nairobi, ambako uchunguzi wa kilichotendeka utafanyiwa ili ripoti
itakayotolewa ibaini iwapo aliwachafua kuku hao au la ni nini hasa
kilichopelekea kifo chake.
Kadhalika,
kamanda huyo alisema nayo mizoga ya kuku hao wawili itapelekwa katika
maabara ya taasisi ya Kabete Veterinary ambako itachunguzwa iwapo
walichafuliwa au la na kilichopelekea vifo vyao.
“Hili ni
suala la uchunguzi, hakuna mtu anayehojiwa, walalamishi wamefariki na
iwapo wangekuwa hai hawangeweza kuongea. Kijana alipelekwa katika ufuo
wa City, Nairobi ambako daktari wa upasuaji ataukagua na atoe ripoti
yake itakayoeleza kila kitu. Pia, chupa ambayo iliokotwa katika nyumba
yake itakaguliwa pia huko,” alisema OCPD huyo.
Bw Opiyo
aliongeza: “Nayo mizoga ya kuku hao, itapelekwa katika Kabete Veterinary
ili ikaguliwe ijulikane iwapo walichafuliwa au la na vifo vyao
vilitokana na nini.”
NA GEORGE MUGO