Wananchi na askari wakitazama Mabaki ya
nyumba ya mshtakiwa wa tukio la Ubakaji wa mtoto wa miaka mitatu, nyumba
ambayo imevunjwa na wananchi, kwa madai ya hasira za wananchi baada ya
mahakama kumuachia kwa dhamana mshtakiwa Chesco Mbwilo.
Mwananchi akichangia mawazo juu ya madhara ya sheria za kuwaachia watuhumiwa wa matukio ya Ubakaji wa watoto.
Wananchi wakiwa katika mkutano wa dharura kujadili suala la kuachiliwa mshtakiwa wa tukio la Ubakaji.
Na Oliver Moto, Iringa
WANANCHI wa kijiji cha Kiwere kilichopo
katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa, wameandamana na kuvunja nyumba
ya Chesco Mbwilo mstakiwa wa kesi ya Ubakaji, kupinga hatua ya Mahakama
kumuachia huru mshtakiwa huyo jambo ambalo wamesema limevunja mahusiano
ya polisi jamii na ulinzi shirikishi.
Akizungumzia mkasa huo wa kuvunjiwa
nyumba na kuiacha familia ya mtuhumiwa yenye watu zaidi ya watano ikiwa
haina makazi, mke wa mshtakiwa huyo amesema wananchi walipofika katika
nyumba yake walimtaka awaonyeshe mumewe na baada ya kumkosa ndipo
wakachukua uamuzi wa kuvunja nyumba.
Wananchi hao walivunja nyumba kubwa ya Bati na kusababisha mali zote za ndani kufukiwa na Tofali, huku wakichoma kwa moto Mkokoteni wa kukokotwa kwa wanyama, pamoja na badhi ya mali na hivyo kuiacha familia hiyo ikiwa haina makazi.
Wananchi hao walivunja nyumba kubwa ya Bati na kusababisha mali zote za ndani kufukiwa na Tofali, huku wakichoma kwa moto Mkokoteni wa kukokotwa kwa wanyama, pamoja na badhi ya mali na hivyo kuiacha familia hiyo ikiwa haina makazi.
Wakizungumzia sababu za kuchukua uamuzi
huo, wananchi hao wamesema hatua hiyo imetokana na watoto wengine watano
kumlalamikia mshtakiwa huyo kuwa amekuwa akiwafanyia ukatili huo wa
ubakaji kwa kuwarubuni kwa Maandazi na Kamera, huku wakielekeza lawama
zao kwa Mahakama, ambayo imetoa dhamana.