

Mwanamuziki staa wa bongo fleva Rehema Chalamila a.k.a Ray C amepotea
katika anga ya muziki kwa kipindi kirefu kutokana na matatizo ya
matumizi ya madawa ya kulevya na baada ya kupata tiba sasa mambo
yanaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida.
Pamoja na ukimya wake katika muziki, Ray C a.k.a kiuno bila mfupa sasa
anaonekana kuwa active zaidi katika mitandao ya kijamii hususan
Instagram.
Ray C ameshare baadhi ya picha na fans wake kupitia instagram
ambazo kwa namna moja au nyingine zinaongea zenyewe (kwa kusindikizwa
na captions) juu ya maisha yake ya sasa. Kwa ufupi ni kuwa Rehema
anakula bata tu sasa hivi, thanks kwa shavu alilopewa na Rais Jakaya
Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’. Take a look….
Hizi ni baadhi ya picha zinazomwonesha yeye mwenyewe alivyo sasa, amenenepa sana!



