Manamba wakiwa kwenye gari la matatu waliloteka na kulazimisha abiria
kutoa nje katika barabara ya Langata Novemba 29, 2012 wakati wa mgomo wa
kupinga sheria mpya za trafiki. Picha/EMMA NZIOKA
IDADI kubwa ya wizi unaofanywa kwenye
magari ya uchukuzi wa umma hufanywa kwa ushirikiano wa madereva na
makondakta, kulingana na polisi.
Mkuu wa Polisi Nairobi, Benson
Kibui, alisema hatua zitachukuliwa dhidi ya wahudumu wa matatu
wanaohusika na vitendo hivyo, na kutaka wamiliki wasaidie katika
kupunguza matukio hayo.
Wasiwasi
ulijitokeza kwenye mkutano baina ya wamiliki wa matatu zinazohudumu eneo
la Eastlands, na polisi wa kituo cha Buruburu, Ijumaa iliyopita.
Bw Kibui aliagiza maafisa wake waandae mkutano huo kufuatia ongezeko la visa hivyo vinavyolenga magari ya uchukuzi wa umma.
Aliongeza kuwa wamiliki watahitajika kupekua wasafiri kabla kuabiri magari, hasa usiku.
Dereva mmoja
anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu kwa “kukosa kuzuia uhalifu”,
baada ya basi alilokuwa akiendesha kuvamiwa, na wasafiri kuporwa mali
yao, kulingana na mkuu wa kituo cha polisi cha Buruburu Benjamin Nyamai.
Ukaguzi
“Tuna sababu
za kushuku dereva huyo alihusika. Alifuata njia aisiyostahili, na
tunashuku alifanya hivyo kuepuka eneo la ukaguzi wa polisi. Alisimamisha
gari mahali ambapo hakustahili kushukisha abiria, na wakati wasafiri
wengine wote wakiporwa, hakuna kilichoibwa kutoka kwake.
Pesa zake na simu hazikuguswa,” alisema.