skip to main |
skip to sidebar
LORI LILILOBEBA MABOMBA YA KUSAFIRISHA GESI LASHAMBULIWA KWA MAWE HUKU DEREVA AKIDAIWA KUJERUHIWA MJINI MTWARA
HABARI
zilizotufikia kutoka mjini Mtwara Zinasema kuwa Gari lililobeba Shehena
ya Mabomba ya Kusafirishia gesi kutoka Mjini Mtwara kuelekea Dar
limeshambuliwa na mawe na kupelekea dereva wa lori hilo Kujeruhiwa
vibaya.
Lori
hilo lilianza kushambuliwa mara baada ya kuingia katika Manispaa ya
Mikinda Mtwara Mjini sababu ya kushambulia gari hilo ni
katika kile kinacho dhihirisha kuwa wanamtwara bado hawajakubaliana na
hoja ya Serikali ya kutaka kusafirisha gesi hiyo kwa ajili ya manufaa ya nchi.
Lori hilo kwa sasa lipo kituo kikubwa cha polisi Mtwara, ikiwa ni
wiki moja tu imepita tokeaa watu kadhaa kukamatwa na jeshi la polisi
mkoani Mtwara kwa kile kinachodaiwa kusambaza waraka wa kuhujumu
miundombinuu yote ya gesi mara tu serikali itakapo anza utekelezaji wake
wa ujenzi wa bomba hilo kupeleka Dar.
Source: Jamii Forum
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi