DIWANI WA KATA YA IWAWA WILAYANI MAKETE AHIMIZA WANANCHI WAKE KUPENDEKEZA KIJIJI KIGAWANYWE

Wananchi wa kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe, wametakiwa kushiriki kikamilifu katika mchakato wa mapendekezo ya kugawa vijiji, na tarafa wilayani hapo, kabla ya julai 20 mwaka huu, ikiwa ni njia mojawapo ya kurahisisha maendeleo ya wananchi

Kauli hiyo imetolewa na diwani wa kata ya Iwawa Benjamin Mahenge wakati akizungumza na mtandao huu kuhusiana na suala hilo

Diwani Mahenge amesema hivi sana serikali imeona adha wanayoipata wananchi, huku akitolea mfano wa kata yake kuwa na kijiji cha Ndulamo ambacho ni kikubwa hivyo wananchi wake wanatakiwa kutoa mapendekezo hayo haraka

"Kijiji cha Ndulamo ni kikubwa sana, hakuna haja ya wananchi wake kuogopa kutoa mapendekezo, tayari nimeshawaambia kuhusu hilo na naimani watalifanyia kazi mara moja ili mapendekezo hayo yafike kunakohusika" alisema Mahenge

Hivi sasa wilaya ya Makete kwa ujumla ipo kwenye mapendekezo ya kugawa vijiji na tarafa kubwa kwa lengo la kurahisisha huduma za wananchi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo