BALOZI WA SUDAN NIGERIA ASEMA RAIS OMAR BASHIR HAKUKIMBIA KUHOFIA KUKAMATWA

BALOZI wa Sudan nchini Nigeria mnamo Jumatano alikanusha habari kuwa rais Omar Al-Bashir alitoroka nchini Nigeria kwa hofu ya kukamatwa, akisema kuwa rais huyo aliondoka baada ya kumaliza ziara rasmi nchini Nigeria.
Akitoa taarifa hiyo mjini Abuja, balozi huyo, Bw Tagelsir Mahgoob Ali, aliwaambia wanahabari kuwa rais huyo alikuwa amepanga kukutana na marais wengine watatu wakiwemo, rais Goodluck Jonathan wa Nigeria, waziri mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegm na rais wa Kenya Bw Uhuru Kenyatta. 

Hili alisema ndicho kilikuwa kiini cha kutokuwepo kwake. Bw Al-Bashir alikuwa nchini Nigeria kwa mwaliko wa Umoja wa Afrika(AU) katika kongamano maalum kuhusu Ukimwi na Malaria.
 
Muungano huo umepitisha azimio linaloyakataza mataifa wanachama kumkamata rais yeyote aliye afisini na anayekabiliwa na mashtaka ya uhalifu wa kivita  katika mahakama ya ICC.

Balozi huyo alisema kuwa ni baada ya kuandaa mkutano katika ubalozi huo ambapo alionelea kurudi nchini Sudan, kwani hakukuwa na jambo lingine muhimu lilikuwepo ambalo lingemfanya kubaki nchini Nigeria kwa siku ya pili.

Aidha, balozi huyo alisema kuwa rais Bashir alimtuma waziri wake wa afya kusoma hotuba kwa niaba yake, huku akifanya mashauriano na marais hao watatu katika vikao tofauti.

Balozi huyo alisema kuwa Bw Bashir hajawahi kuwa na wazo lolote la kuogopa kukamatwa akiwa nchini Nigeria, huku akiongeza kuwa Nigeria ilikuwa mojawapo  ya mataifa  yaliyopinga ubaguzi wa ICC barani Afrika.” Ikiwa Nigeria ingeusikiza wito wa ICC, ingejitokeza vipi kama mojawapo wa nchi zinazopinga mwingilio wake barani Afrika,” akasema Bw Ali.

Kando na hayo, alionya kuwa ikiwa Al- Bashir 'angeanguka’, ni kama bara la Afrika limeanguka. Balozi huyo alisema kuwa Afrika sharti ikatae juhudi za nchi za Kimagharibi kuleta  ukoloni mamboleo. Alisema kuwa mahakama ya ICC imekuwa fimbo ya kisiasa, na kwa hivyo mataifa ya Afrika sharti yaikatae. Alitia shaka 'kujitolea’ kwa nchi za Magharibi katika kukabiliana na Ukimwi na Malaria.

NA AFP


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo