WANANCHI WA MAKETE MKOANI NJOMBE WAASWA KUTUNZA MAZINGIRA

Msitu wa Ipuji uliopo wilayani Makete kama unavyoona unatunzwa vizuri
Msitu huo wa Ipuji ambapo hapa baadhi ya watu waliharibu mazingira yake
Utupaji taka ovyo kama unavyoonekana katika kitongoji cha Kona Makete mjini
Katibu tawala wilaya ya Makete Joseph Chota akisoma hotuba ya siku ya mazingira kwa mwaka huu katika kwa niaba ya mkuu wa wilaya Josephine Matiro, katika kata ya Isapulano wilayani Hapa
-----------

Wananchi wilayani Makete wametakiwa kuhakikisha kuwa wanahifadhi mazingira kwa kuwa ni jambo muhimu ambali litasaidia kuona raha ya kuishi kutokana na mazingira hayo kuzidi kuwa mazuri

Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine Matiro katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na katibu tawala wilaya hiyo Bw. Joseph Chota katika maadhimisho ya siku ya mazingira duniani yaliyoadhimishwa kiwilaya katika kata ya Isapulano

Amesema utunzaji wa mazingira ni jambo zuri na la umuhimu hivyo kuwataka wananchi kutambua umuhimu huo wa kuhifadhi mazingira, ikiwa ni pamoja na kutokata miti ovyo, kutupa taka ovyo pamoja na shughuli zote ambazo zinaharibu mazingira

Matiro amesema ujumbe wa mwaka huu unasisitiza kupunguza matumizi ya rasilimali zisizo rafiki na mazingira pamoja na kupunguza au kuepuka uchafuzi wa mazingira, huku akisistiza kuwa wananchi wakikubali kubadilika mazingira ya makete yatazidi kuwa mazuri siku hadi siku

Kwa upande wao idara ya maliasili wilaya ya Makete imesema jutihada zinaendelea kufanywa na idara hiyo kuhusu utunzaji wa mazingira ambapo wanaendelea kutoa elimu kuhusu kulinda na kuhifadhi vyanzo vya maji pamoja na kupanda miti ambayo ni rafiki na mazingira ikiwemo Mivengi na Mitulunga

Wamesema kwa msimu wa mwaka 2012/2013 zaidi ya miti laki 8 imepandwa wilayani Makete huku lengo la wilaya lilikuwa ni kupanda miti milioni 9 na wameshindwa kupata uhakika kama lengo hilo limefikiwa kutokana na baadhi ya kata 6 ikiwemo Isapulano ambayo maadhimisho hayo yamefanyika, kushindwa kufikisha taarifa za upandaji miti kwenye ofisi ya maliasili na mazingira kwa wakati, ila wanaamini lengo hilo limefikiwa

Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani huadhimishwa kila tarehe 5, Juni ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni fikiri kabla ya kula, hifadhi mazingira


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo