Huyu ni miongoni mwa mtuhumiwa wa wapiga nondo katika mkoa wa IRINGA akipokea
kichapo kikali huku akiwa chini ya ulinzi mkali kuelekea kituo cha
polisi, jamaa huyu anayefahamika kwa jina la MASTER, Amekamatwa mara tu
baada ya mwenzake kukamatwa leo hii asubuhi akidaiwa naye kuhusika na
uhalifu huo. hii imetokea mara tu baada ya matukio ya namna hiyo
kuripotiwa mara kwa mara siku za karibuni
Baadhi
ya wananchi mkoani IRINGA wakiwa na hasira na kutembeza kichapo kwa
mhalifu huyo kwa kua wamechoshwa na matukio hayo yaliyokithiri mkoani hapo
Mtuhumiwa akiwa katika hali ngumu maana wananchi wana hasira sana na
watu wa namna hiyo kuwafanyia unyama kwa kuwapiga nondo na kuwapora mali
zao
Wananchi wakiwa hawaogopi askari wakiendelea kumpa kichapo mtuhumiwa wa uhalifu huyo huku safari ya kuelekea kituoni ikiendelea
Watu wakiwa wengi kusaka na kuwakabidhi watuhumiwa hao mikononi mwa polisi
Wananchi wakishangaa kilichojiri leo mjini IRINGA
Picha na Peter Sanga