Wanachama
wa chama cha mapinduzi tawi la Ikonongo kata ya mkwawa manispaa ya
Iringa wamefanya harambee kwa ajili ya kukomboa kiwanja ambacho
walitakiwa kujenga ofisi ya chama chao.
Akizungumza
katika harambee hiyo Mwenyekiti wa tawi AMRI KALINGA amesema kuwa
ujenzi huo umeshindwa kufanyika mapema kutokana na kiwanja hicho kuwa na
mgogoro ila kwa sasa wameshafikia muafaka na tayari wamelipa fidia ya
shilingi laki tano na nusu.
Naibu
meya wa manispaa GERVAS NDAKI ambaye alikuwa mgeni rasmi katika harambee
hiyo amewataka wananchi hao kuwa wabunifu kwa vitu ambavyo vitawasaidia
kuwainua kiuchumi katika kijiji chao na sio kuishia kujenga ofisi.
