Naibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu imesema
serikali inaanda oparesheni maalumu ya kupambana na watu wanaojihusisha na vitendo
vya ujangili katika hifadhi za taifa kwa kuwa vinatishia hali ya usalama wa
nchi.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa mkutano wa wadau wa
Ulinzi wa Maliasili katika hifadhi za
taifa zilizopo mikoa ya nyanda za juu kusini Nyalandu alisema vitendo vya
ujangili hususani vinavyohusisha na
uwindaji haramu na uuaji wa Tembo vinatisha kutokweka kwa wanyama hao nchini.
Alisema tafiti zilizopo zinaonesha kuwa kwa sasa Tembo 10,000
wanauawa katika kila mwaka hapa nchini na
kuongeza kuwa idadi hiyo ni kubwa na kama itachwa iendelee Tembo waliopo nchini
ambao wanafikia 140,000 watatoweka.
“Serikali imeweka mkakati malaumu wa kupambana na vitendo
hivyo,kwanza tunafanya mabadiliko makubwa katikasheria zetu suala zima la utoaji adhabu
kwa watu watakaobainika kujihisha na vitendo hivyo…wito wangu kwa wanachi wanajihusisha na kazi hiyo kuacha mara moja na
watu wote kushiriki katika shughuli za
ulinzi wa Maliasili za Taifa”alisema Nyalandu.
Nyalandu alifafanua kuwa vitendo vya ujangili katika maeneo
ya hifadhi kwakiwango kikubwa vinatekelezwa na watu ambao hushirikiana na watumishi katika idara
mbalimbali za serikali na mamlaka zinazofanya kazi katika hifadhi hizo na
kuongeza kuwa katika mkakati ulipo kila atakayebainika kuanzi sasa atatangazwa
hadharani na kuchukuliwahatua kali bila kujali wadhifa wake.
Alitaja makundi ya watu wanaofanya kazi katika maeneo ya
hifadhi za Taifa,Viwanja vya Ndege,Bandarini na idara za uhamiaji walioko katika
maeneo ya mipakani kuwa baadhi yao wanaoshiriki katika vitendo hivyo vya ndiyo
sababu pembe za ndovu kutoka hapa nchini husafirishwa hadi nje ya nchi bila ya
kukamatwa .
“Isingewezekana mtu aingie kwenye hifadhina kuoa Tembo hadi
anafiisha idadi ya meno yanye kujaza loli kisha afukie chini na kutafuta gari
la kubeba Meno hayo bila ya kujulikana,mtu huyo ni lazima ashirikiane na baadhi
ya watu katika makundi haya, …,natoa wito kwa wafanyakazi katika hifadhi za
Taifa,viwanjwa vya Ndege,Bandarini na wale walioko mipakani kuacha kushirikiana
na majangili kwani watakaobainika serikali hawaitawahurumia”alisema Nyalandu.
Alitaka watu wote
wanaomiliki silaha kinyume na sheria za nchi kuzisalimisha kabla ya mchakato na
hatua kali za kisheria hazichukuliwa dhidi yao kwa kuwa silaha hizo haramu
zimekuwa zikitumika katika kutekeleza vitendo vya uharifu katika hifadhi za
Taifa.
Kuhusu majangili kutumia silaha kali alisema serikali
inafanya majadiliano na nchi mbalimbali kuona njia sahihi za kupambana na
majangili hao kwa lengo la kunusuru wanyama hao hususani Tembo ambao kwa sasa
idadi yao imepungua sana.
Nyarandu alitajasababu za kukithiri kwa vitendo vya uhalifu
huo kuwa zinatokana na ongezeko la matumizi ya pembe za Ndovu na soko kubwa
lililopo katika baadhi ya nchi hususani za bara la Asia.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Tanapa Taifa Alan
Kijazi alisema mkutano huo ulioandaliwa na Mradi wa kuboresha Mtandao wa Ulinzi wa Hifadhi za
malisili katika mikoa ya Nyanda za Juu
Kusini umelenga kukusanya maoni ya namna ya kupambana na ujangili kufutia
oongezeko la ujangili katyika hifadhi za Taifa.
Alisema mkutano huo wa siku mbili utajadili hatua za
kuchukua katika kupambana na vitendo hivyo na kisha kuunda kikundi kazi kwa
ajili ya kukabiliana na vitendo vya ujangili katika hiafadhi zilizpo katika miko
ya nyanda za juu kusini.
Mkutano huo ulihudhuriwa na wakuu wa mikoa kutoka mikoa ya
Nyanda za juu kusini na pia na wakuu wa wilaya zote toka katika maeneo hayo.
Na Berdina Majinge, Iringa
