Moto mkubwa umezuka jana na kuunguza chumba kimoja katika maeneo ya kibwabwa Ipogolo kata ya Ruaha manispaa ya Iringa.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa
iringa RAMADHANI MUNGI amesema moto huo umezuka katika nyumba
ya HIRALI RAMADHAN ambayo ilikuwa na wapangaji.
Amesema
chumba hicho kilikuwa kinakaliwa na CHRISTINA MFUGA na moto huo haukuwa
na madhara yoyote kwa binadamu kwani kikosi cha zima moto kiliwahi
kufika katika eneo la tukio.
Aidha
amesema kuwa jeshi la polisi bado linaendelea kufanya uchunguzi ili
kubaini chanzo cha moto huo pamoja na gharama za vitu ambavyo
vimeteketea.
WAKATI HUO HUO.
Mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la JOJINA KABOGO(29) anashikiliwa na
jeshi la polisi mkoani Iringa kwa uchunguzi zaidi kufuatia tukio la
kuokotwa kwa mtoto mchanga mkoani hapa.
Tukio
hilo limetokea katika maeneo ya mlandege manispaa ya iringa
ambapo afisa mtendaji wa mtaa huo FADHILI OSKA amemuokota mtoto huyo
anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi 6 jinsi ya kiume akiwa ametupwa
jalalani.
Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa iringa RAMADHANI MUNGI amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi bado unaendelea na kosa hilo
ni la jinai, na ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa iringa kuacha tabia
hiyo