MKUU WA MKOA WA MOROGORO AFIKA KUTOA POLE NYUMBANI KWA MANGWEA

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera akiwasili nyumbani kwa Mama mzazi wa Mangweha.
Mama Mzazi wa Mangweha, Denisia Mangweha akiwa nyumbani kwake kabla ya safari kuelekea Uwanja wa Jamhuri.
Denisia Mangweha akiwa na binti yake mkubwa Magreth Mangweha.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera Leo asubuhi amefika nyumbani kwa Mama Mangwea eneo la Kihonda Mazimbu Road na kumpa pole kwa niaba ya wakazi wote wa mkoa wa Morogoro. 

Baada ya kutoa pole, Mhe. Bendera aliongoza umati wa watu kutoka Kihonda kuelekea Uwanja wa Jamhuri kwa shughuli za kuaga mwili wa Albert Mangweha aliyefariki dunia Mei 28 mwaka huu nchini Afrika Kusini. 

Mangweha anatarajiwa kuzikwa katika makaburi ya Kihonda nje ya Kanisa la Mtakatifu Monica jirani kabisa na alipozikwa baba yake mzazi Mzee Keneth Mangweha.
(Picha zote na Dustan Shekidele / GPL)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo