MBUNGE WA MTWARA MJINI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA UCHOCHEZI VURUGU ZA MTWARA


Mbunge wa Mtwara Mjini, Hasnein  Murji (pichani) ametiwa mbaroni na Jeshi La Polisi kwa tuhuma za uchochezi na  kuhusika katika vurugu zilizotokea hivi karibuni katika viunga vya mji wa Mtwara.

Habari zilizoifikia blog hii usiku huu zimeeleza kwamba mbunge huyo amekamatwa saa 2:30 usiku huu na anashikiliwa katika kituo Kikuu cha Polisi Mjini Mtwara.

Katibu wa Mbunge huyo Meckland Millanzi amethibitisha kukamatwa kwa Murji na kwamba anahusishwa na mvurugu hizo.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso  amesema kwamba Murji amekamatwa usiku huu nyumbani kwake katika eneo la Shangani.

Taarifa zimebainisha kwamba Murji amekamatwa na kwamba hati ya kumkamata imeeleza anatuhumiwa kuchochea vurugu za kupinga gesi ya Mtwara kwenda jijini Dar es Salaam.

Mpaka sasa watu zaidi ya 80 wamekamatwa na jeshi la polisi na kushtakiwa mahakamani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo