MAJONZI TENA:MSANII KHADIJA KOPA AFIWA NA MUMEWE

Taarifa nilizozipata mapema leo alfajiri zinasema kwamba Mume wa Malkia wa Mipasho,  Bi. Khadija Kopa, aitwaye Jaffari Ally amefariki dunia usiku wa kuamkia leo majira ya saa 9 usiku, Katibu wa Bendi ya TOT Gasper Tumaini amethibitisha juu ya msiba huo.
Taarifa za awali zinasema kwamba chanzo cha kifo chake ni ugonjwa wa Malaria, ambapo siku ya Jumatatu marehemu Ally alipelekwa Hospitali ya Lugalo kwa ajili ya kupata matibabu.


Taarifa zaidi zinasema kwamba marehemu alipata nafuu na kurudi nyumbani kwao Bagamoyo, hali ambayo ilimpelekea Khadija Kopa kusafiri kikazi, na inasemekana mpaka umauti unamkuta Jaffari, Mkewe Khadija Kopa alikuwa yupo kikazi mikoani kwa ajili ya shughuli zake za kimuziki.


Pole sana Bi. Khadija Kopa kwa kumpoteza Mumeo Mpendwa, Mungu akutie nguvu katika kipindi hiki kigumu. 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo