MAHAKAMA YAAMURU SHULE IUZWE MBEYA

 Hii ndiyo Shule ya Msingi ya Besta Sae Mbeya.
Vibarua waliopewa jukumu la kuhamisha mizigo shuleni hapo
 Viti  vikiwa vimetolewa eneo la shule ya Msingi Besta
 Wanafunzi wa Shule ya Msingi wa Besta wakiwa wanakusanya Madftari yake pamoja na Mitihani yao.
 
Na Ezekiel Kamanga
Mahakama kupitia dalali wa Mahakama imepiga mnada Shule ya Msingi Besta iliyopo Sae jijini Mbeya kutokana na madai ya mdai katika kesi hiyo .
 
Mdai wa kesi hiyo namba 212 ya mwaka 2003 ni Kampuni ya Mohamed Enterprises ambapo alikuwa anamdai Hamis Othman kiasi cha Shilingi Milioni 270 ambazo alishindwa kulipa . Kesi hiyo namba 27 ilianza kusikilizwa mwaka 2003 huku Othman  akitetewaa na Wakili Mkumbe ambapo hukumu ilitolewa 4.6.2012  majengo ya shule yauzwe, mpaka sasa madai hayo  hayaja jurikana yalikuwa yanahusiana na nini.
 
Wamiliki wapya wa majengo  hayo ni Mbeya Heritage Company ambao walikabidhiwa majengo hayo na Dalali wa Mahakama Chini ya usimamizi wa mtendji kata ya Ilomba Erasto Mwakapoma  na Mwenyekiti waa Mtaa wa Sae Erias Mwakyusa huku  Jeshi la Polisi Likishuhudia makabidhiano hayoyakifanyika kwa amani.
 
Zoezi lilisitishwa kwenye Msikiti kutokana na Imani waumini wa Msikiti huo wataalifiwe ili ndani ya siku Mbili wawe wameondoka eneo hilo. 
 
Adha kubwa ilikuwa ni kwa wanafunzi wliokuwepo shuleni hapo ambapo mitihani yao ilioekana kuzagaa hovyo kutokana  na purukushani zilizo kuwepo bila taarifa yoyote na kutojua Hatma yao  ya masomo yao kutokana na Madarasa kuhodhiwa  na mmiliki mwengine Licha ya kuwepo kwa mabweni kando ya Shule hiyo na kufanya mizigo yote kulundikwa nje ya mabweni.

Picha na Mbeya yetu Blog


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo