Mwanalibeneke
Othman Michuzi a.k.a "Mzee wa Mtaa kwa Mtaa" wa Kampuni ya Michuzi
Media Group juzi kati alitinga ndani ya Hafla ya Utoaji wa Tuzo za
Muziki za Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013,zilizokuwa zikitolewa
katika ukumbi wa maraha na burudani pale Mlimani City,Jijini Dar.
Alichokifanya
mwanalibeneke huyo Othman Michuzi kwa kutumia kamera yake au Jicho
Kubwa lionalo mbali,ni kurekodi matukio mbali mbali ya usiku huo
zikiwemo video za matukio,ambapo video hizo zinawezekana zikawa ndio
tiketi ya kuupeperusha muziki wa Tanzania katika masoko ya kimataifa,
labda wengi walistushwa na kiwango cha juu cha kimataifa katika video
hii https://www.youtube.com/watch?v=ZDcmpDoZQZM
Wataalamu
wa masoko wa kimataifa waliotazama video hiyo katika Youtube,wameshauri
kuwa itakuwa jambo la busara kwa Kampuni ya Michuzi Media Group,
Kuhifadhi haki yake katika video hizo, na mameneja wa wasanii au bendi
wakae meza moja na menejmenti ya Michuzi Media Group,ili wakubaliane
kutumia Bidhaa hiyo kuwa Demo ya kuwapromoti wasanii au bendi zao
Duniani.
Kuzitumia
bila ya ridhaa ya aliepiga video hizo ni kinyume cha sheria. Kukopi na
kupesti bila ya Idhini au ridhaa ya walipiga video hiyo ni kuvunja
sheria na heshima.
ni
Ushauri tu, lakini Hongera nyingi sana sana kwa Mpiganaji Othman Michuzi
kutoka kwa wadau wa ughaibuni,kwani Kazi aliyoifanya imeipeperusha
vyema Bongo yetu Kimataifa endelea kwa kasi hiyo hiyohttps://www.youtube.com/watch?v=lZYxySYLmI
Unaweza tembelea libeneke lake kwenye link hiyo http://othmanmichuzi.blogspot.com
Pia unaweza tembelea ukurasa wake wa youtube kwa link hii https://www.youtube.com/user/Michuzijr2?feature=watch ili kuona video mbali mbali.
Mdau Msema Kweli
Ughaibuni.
