Kikosi
cha zima moto kimeendelea kutoa elimu juu ya umuhimu wa kinga na
tahadhari ya moto katika meneo mbalimbali ya makazi ya watu ikiwemo
sehemu ya kuufanyia biashara.
Akizungumza
Kamanda wa kikosi cha zimamoto mkoa wa Iringa KENEDY KOMBA, amesema
kuwa lengo la kufanya hivyo ni kuondoa kero kwa wananchi ili wafahamu ni
kitu gani wanalipia pamoja na manufaa yake.
Amesema zoezi hilo hufanyika kila mwaka wa fedha wa serikali kuanzia julai 1 mwaka husika mpaka mwaka unaofuata juni 30.
Aamesema
kuwa mbali na kutoa elimu pia kuanzia tarehe 1 mwezi wa kumi mwaka jana
walikuwa wakifanya zoezi hilo pamoja na ukusanyaji wa madhuhuri ya
serikali na muda wake umekwisha na kwa wale wote watakaokuwa
hawajakamilisha sheria itachukua mkondo wake.
Aidha
amesema kuwa kwa wale ambao hawajafikiwa wafike wenyewe katika ofisi ya
kamanda wa zimamoto na kwa wale ambao wamefikiwa na wamepewa hati ya
malipo wanapaswa kufahamu kuanzia sasa ndani ya siku saba watafikishwa
mahakamni.
Kwa
upande wa wamiliki wa vyombo vya usafiri amesema kuwa kodi yao inakatwa
kupitia TRA na baada ya kukatwa pesa hizo wanatakiwa kufika katika ofisi
ya kamanda wa zimamoto na uokoaji ili kukaguliwa na kupewa ushauri
vifaa gain vinafaa kuwekwa katika vyombo hivyo na namna ya kutumia
vyombo hivyo na ili kuthibitisha kama umekaguliwa unapewa fomu maalum.
