WADAU
TUNAOMBA RADHI KWA PICHA HII KAMA ITAKUKWAZA LAKINI NDIO UNYAMA WA
BINADAMU WA SASA….KUNA WANAOKESHA USIKU KUCHA WAKIMLILIA MUNGU AWAJALIE
KUZAA LAKINI WENGINE WANATUPA WATOTO WASIOKUWA NA HATIA…Pichani ni Maiti ya kitoto kichanga ikiwa kwenye
mfuko wa rambo.
Wakazi wa eneo la Magomeni
zilipovunjwa nyumba za KOTA jijini Dar es salaam leo wakishuhudia mtoto
mchanga anayekadiriwa kuwa umri wa siku moja akiwa ametupwa huku akiwa
amekufa katika eneo hilo na mtu asiyefaamika. (Picha na Philemon Solomon
wa Fullshangwe).
Gari
la askari polisi wa kituo cha Magomeni usalama wakiwa katika eneo
ambalo ametupwa mtoto mchanga akiwa amekufa kwa ajili ya kuchukua mwili
wake na kumpeleka sehemu husika.
Maiti ya Kitoto kichanga kinachokadiriwa kuwa na umri wa siku moja ikiwa imepakiwa kwenye gari la polisi.
Wakazi wa jirani na eneo hilo wakiwa wamekusanyika eneo la tukio. (Picha na Mo Blog)