Habari
kutoka ndani ya Jeshi la Polisi nchini zinasema kuwa Mwenyekiti wa
Jumuiya ya Vijana wa Chama cha CUF, Katani Ahmed Katani, ametiwa nguvuni
jijini Dar es Salaam akituhumiwa kuhusika na uchochezi wa vurugu ambazo
zimekuwa zikitokea mkoani Mtwara.
Katika
kutafuta ukweli wa habari hii Mwandishi wetu aliwasiliana na
viongozi kadhaa wa CUF, akiwemo Julius Mtatiro ambaye ni Naibu Katibu
Mkuu wa CUF, ambao walithibitisha kukakamatwa kwa Bwana Katani na kuwa
tayari amekwishasafirishwa kwendaMtwara.
Taarifa
kutooka ndani ya chama cha CUF zimethibitisha zaidi kuwa Katani
alipigiwa simu na maofisa wa polisi wa Kituo Kikuu na kuelezwa kuwa
anatakiwa afike kituoni hapo kwa mahojiano ambapo mara baada ya kufika
alitiwa nguvuni na kuanza kuhojiwa.
Itakumbukwa
kwamba ni muda mrefu sasa kumekuwa kunatokea vurugu Mtwara
zinazohusiana na wananchi kupiga mradi wa bomba la gesi kutoka mkoani
humo kwenda Dar es Salaam. Hadi sasa vurugu hizo zimesababisha vifo vya
watu na uharibifu wa mali za serikali, viongozi na raia.
Kufuatia
matukio hayo serikali ilitangaza kuwasaka watu wote watakaothibika
kuhusika na vurugu hizi ambazo kwa ujumla zinaitia doa nchi yetu.
credits dar24