ATUMBUKIA MTONI NA KUFA KUTOKANA NA ULEVI

KIJANA mmoja Evasto Jamshindi (19) mkazi wa kijiji cha Ndola kata ya Mwaya wilayani Kyela amekufa baada ya kutumbukia kwenye mto Mbaka alipokuwa akivuka kwenye daraja la miti akiwa na baiskeli na hii ilitokana na kunywa pombe nyingi kuzidi kiasi

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo mwenyekiti wa kijiji hicho cha Ndola  Teddy Mwakapyela ni kuwa kijana huyo aliangukia mtoni siku ya alhamisi wiki iliyopita majira ya saa tatu usiku alipokuwa akitoka ulevini katika kijiji cha Ilopa akiwa na mwenzake Mark Mwanyalala na zoezi la kumtafuta marehemu ilidumu kwa muda wa siku nne

Alisema kuwa baada ya taarifa kufika kijijini kwao juu ya hilo wao walitoa taarifa polisi na kuanza msako wa kuutafuta mwili wa marehemu majini hadi katika ziwa Nyasa wakidhani kuwa huenda maji yakawa yamempeleka huko lakini bila ya mafanikio


Mwenyekiti huyo wa kijiji alisema kuwa jana majira ya saa nane mchana walipata taarifa kutoka kwa raia wema baada ya kuuona mwili wa binadamu ukielea majini katika mto mbaka na ndipo walipokwenda kuutizama na kuuona kuwa ndiyo ule mwili wa marehemu waliokuwa wakiutafuta  na kwenda kutoa taarifa polisi

Alidai kuwa baada ya kuuopoa mwili wa marehemu majini waliukuta mwili huo ukiwa na baadhi ya majeraha ambayo yalianza kuwapatia maswali ya nini kilichopelekea mwili huo kupata majeraha

Mganga aliyeufanyia uchunguzi mwili huo wa marehemu Nsubiri Mwansule alisema kuwa kifo cha marehemu kimetokana na kunywa maji mengi baada ya kutumbukia majini na kuwa mpaka jana walipomuokoa majini alikua akitoka maji mengi kutoka tumboni

Alisema majeraha ya marehemu waliyoyakuta mwilini yalitokana na msukumo wa maji yaliyopelekea kujigonga kwenye mawe na visiki na kuwa kwa jinsi alivyokuwa amelewa ilikua ni ngumu kwake kuweza kupambana na kasi hiyo ya maji ambayo yalikua yakienda kwa kasi

Na Ibrahim Yassin


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo