TAZAMA AJALI MBAYA YA LORI DAR, PRADO NYANG'ANYANG'A

Lori la mafuta likiwa limelidondokea gari ndogo baada ya kutoka ajali katika eneo la Chang'ombe jinini Dar es salaam ikihusisha na daladala ya abiria.
 
  Ajali mbaya inayohusisha Lori la Mafuta, Daladala pamoja na Gari aina ya Prado imetokea muda mfupi uliopita maeneo ya Chang'ombe Machinjioni kwenye mataa Jijini Dar es Salaam baada ya dereva wa dalalala ambayo haikuwa na abiria kuingia vibaya katika makutano ya barabara na kusababisha dereva wa lori kugonga daladala na kuangukia Prado hii wakati akijaribu kukwepa kusababisha madhara.
 
 Hakuna mtu yoyote aliyepoteza maisha katika tukio ili isipokuwa majeraha ya kawaida yamewapata madereva husika, Wananchi wameonekana eneo la tukio wakichota mafuta ya mawese yaliyomwagika kutoka kwenye lori lililopata ajali na mpaka sasa hatua zote za tahadhari zimeshachukuliwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo