TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI YAKATALIWA LUPEMBE NJOMBE

Diwani wa Kata ya Lupembe Bi Twilumba Wapalila katikati Amesema Baada ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo Sasa Mkutano Mwingine Utafanyika Jumamosi Wiki Ijayo.
Katikati ni Diwani wa Kata ya Lupembe Bi.Twilumba Wapalila[Picha wakati wa Baraza la Madiwani toka Maktaba yangu.]
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Wilaya ya Njombe Bwana Lupyana Fute[Jacky's]Aliyevalia Shati la CCM Ambaye Pia ni Diwani wa Kata ya Njombe Mjini awali aliuagiza uongozi wa Kijiji kuwasomea Wananchi Taarifa ya Mapato na Matumizi Kila baada ya Miezi Mitatu Jambo ambalo halitekelezeki.
 
Na Michael Ngilangwa.
Wananchi wa Kijiji Cha Lupembe Barazani Wilayani Njombe Wameikataa Taarifa ya Mapato na Matumizi Iliosomwa na Uongozi wa Kijiji Hicho Wakati wa Mkutano Uliofanyika  Kijijini Humo,Kwa Madai ya Taarifa Hiyo Kuwa na Mapungufu Mengi.

Miongoni Mwa Mapungufu Hayo ni Pamoja na Taarifa Hiyo Kutoaninisha Kikamilifu Kuhusu Matumizi ya
Fedha Za Kijiji Pamoja na Wananchi Kutokubaliana na Mchanganuo wa Fedha Hizo Kama Ulivyoaninishwa na Viongozi Wakati wa Mkutano Huo.

Aidha Kutokana na Hali Hiyo,Uongozi wa Kijiji Ulilazimika Kurudisha Kiasi Cha Shilingi Millioni Mbili Ambazo Hazikuweza Kupatiwa Majibu ya Kina Licha ya Wananchi Kuhoji Mara Kadhaa Kuhusu Fedha Hizo Ambazo Zilitengwa Kwaajili ya Kuboresha Miundombinu ya Maji.

Akizungumza na blog hii ,Diwani wa Kata ya Lupembe Bi Twilumba Wapalila Amesema Baada ya Kuahirishwa Kwa Mkutano Huo Sasa Mkutano Mwingine Utafanyika Jumamosi Wiki Ijayo na Kuongeza Kuwa Wanatarajia Kuzisoma Taarifa Zote Kama Ilivyoelekezwa na Wananchi na Viongozi Mbalimbali wa Chama na Serikali.

Akiwa Kwenye MKutano wa Hadhara Wakati wa Ziara ya Kutembelea Vijiji Vya Tarafa ya Lupembe,Mjumbe wa NEC Taifa Wiilayani Njombe Bw Lupyana Fute Aliuagiuza Uongozi wa Kijiji Hicho Kuhakikisha Unawasomea Wananchi Taarifa za Mapato na Mtaumizi Hadi Kufikia May 18 Mwaka Huu na Kusema Kinyume na Hapo Hatua za Kisheria Zingeweza Kuchukuliwa Kwa Viongozi Hao

Kumekuwa na Hali ya Viongozi wsa Vijiji Mkoani Njombe Kukiuka Sheria za Serikali za Mitaa Zinazowataka Kuwasomea Wananchi Taarifa za Mapato na Matumizi Kila Baada ya Miezi Mitatu Jambo Ambalo Limekuwa Likisababisha Migogoro ya Mara Kwa Mara Baina ya Wananchi na Viongozi Wao.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo