RC IRINGA AKANUSHA TAARIFA ILIYOTOLEWA NA TV MOJA HAPA NCHINI

SERIKALI mkoa  wa Iringa imepinga vikali taarifa  za upotoshaji zilizotolewa na  kituo  kimoja  cha TV hapa nchini  kuhusu kuwepo kwa maandamano  ya wakulima  wa mpunga Pawaga  ambao wanapinga  ushuru wa mazao na kuwa habari hiyo haikuwa na ukweli kwani  waliofanya maandamano hayo ni  wafanyabiashara  wa mpunga ambao  walivaa kofia za wakulima ili kuendelea  kuwanyosha  wakulima.

Akizungumza na  wanahabari leo  ofisini kwake mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dkt Christine Ishengoma  alisema  kuwa kituo hicho cha   Runinga maarufu hapa nchini (jina  tunalo) kilitangaza habari  za  kupotosha  umma kuwa  wakulima  wa mpunga  pawaga  wameandamana hadi ofisi  ya Halmashauri ya  wilaya  Iringa kupinga ushuru  mkubwa wa mpunga jambo ambalo si kweli.

Alisema  kuwa  waliofanya maandamano hayo hawakuwa  wakulima bali  wakuliwa  wafanyabiashara  wa mpunga waliopo mjini Iringa kwa  lengo la kuidanganya serikali kama ni  wakulima  wakati si kweli.

Kwani alisema  kuwa  lengo la wafanyabiashara hao ni kutaka  kuendelea  kuwanyonya wakulima na sio vinginevyo na  hivyo  kuwataka  wanahabari kuwa makini katika  kuandika habari na  kuwa kabla  ya kutangaza  basi kufanya uchunguzi  wa kina ili  kuwa na usahihi  badala ya  kutoa habari za  kupotosha umma.

Dkt Ishengoma  alisema kutokana na maandamano hayo vyombo  vya   usalama  mkoani hapa vimewahoji  wafanyabiashara  hao na kukubali  kudanganya  umma kuwa wao ni  wakulima wa mpunga .

Hivyo  alisema hatua ambazo  zimechukuliwa kwa  wafanyabiashara  hao   ni pamoja na  kutakiwa  kulipa  ushuru na  kuwa hatua  nyingine  za kisheria zitachukuliwa dhidi  yao kwa tukio  hilo.

Hata  hivyo  alisema  kuwa hakuna  mkulima ambae amekuwa akitozwa ushuru kwa zao lao la mpunga na  kuwa ushuru uliopo ni kwa  wafanyabiashara  na  si mkulima.

Pia  mkuu  huyo  wa  mkoa aliwataka  wakulima  mkoani hapa  kuwa makini na mbinu chafu za  wafanyabiashara  katika  uuzaji  wa mazao yao ikiwa ni pamoja  na kuzingatia vipimo  halali  katika  kuuza mazao badala ya  kuuza mazao yao kwa matakwa ya  wanunuzi ya  kutumia vipimo vya lumbesa ambavyo  vimepigwa marufuku mkoani  Iringa.
 
(Na Francis Godwin)


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo