|
BENDI
ya Mashujaa imetangazwa kutoa burudani katika shindano la Redds Miss
Kibaha 2013 shindano lililopangwa kufanyika Mei 17 katika ukumbi wa
Container Mailimoja Kibaha.
Kwa
mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa
Kampuni ya Linda Media Solution (LIMSO) Khadija Kalili ilisema kwamba
tayari wamemalizana na uongozi wa bendi ya Mashujaa hivyo ndiyo
burudani itakayorindima na kuwasindikiza wanyange wa Redds Miss Kibaha.
“Uteuzi
wa bendi ya mashujaa umekuja baada ya kufanya utafiti wa kina juu ya
burudani ambayo itakidhi kiu kwa wakaazi wa Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa
ujumla hivyo kura nyingi likwenda kwa bendi ya Mashujaa naamini siku
hiyo mabo yatakuwa bambam” alisema Kalili.
Kalili
aliendelea kwa kusema kuwa naifahamu vema bendi ya Mashujaa ambayo
inaongozwa na mwanamuziki nyota nchini Charles Mbwana ‘ Charlz Baba ,
Kingunge’ , pia wamo waimbaji wenye sauti tamu kama Jado FFU, Marapa
machacharikama 33, Fagurson na wengineo wengi.
Akizungumzia
kwa upande wa maandalizi Kalili alisema kuwa yanaendelea vizuri huku
LIMSO wakijipanga kuingia kambini na warembo ambako watakaa kwa siku
chache kabla ya shindano.
Shindano
hilo limedhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kwa kupitia kinywaji
chache cha Redds Premium Cold, Maji Umoja, Shear Illusions, Fredito
Entertainment, CXC Africa, Multichoice DSTV,Clouds FM , Times FM Michuzi
Media Group (MMG),Mikopo Finance,Santorine ,PR.Promotion, Chicago
General Company, Image Pub na wadhamini kutoka Kibaha ni Mama Koka ,
Amazon Night Club, Panandipanandi Pub na Santorine Holid
|
MASHUJAA BAND KUSINDIKIZA REDDS MISS KIBAHA 2013
By
Unknown
at
Sunday, May 05, 2013
