Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokea sehemu ya
vifaa vya michezo vyenye thamani ya Sh. Milioni 35, kwa ajili ya vijana
wa Haraiki ya Mbio za Mwenge utakaowashwa Visiwani Pemba Mei 6, mwaka
huu, kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB,
Domina Feruzi, wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika Ofisini kwa
Makamu, Ikulu jijini Dar es Salaam, jana Mei 2, 2013. Kushoto ni Meneja
wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa benki hiyo, Elieza Msuya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wageni
wake kutoka Benki ya NMB, baada ya makabidhiano ya vifaa vya michezo
vyenye thamani ya Sh. milioni 35 kwa ajili ya vijana wa Haraiki wa mbio
za Mwenge unaotarajia kuwashwa Mei 6, mwaka huu Visiwani Pemba.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya
pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa Benki ya NMB, Domina
Feruzi (wa pili kulia) Meneja wa Kitengo cha Huduma za Serikali wa
benki hiyo, Elieza Msuya (kulia) Ofisa Mahusiano wa benki hiyo, Doris
Kilale (wa pili kushoto) na Huruma Mwaihomba, Ofisa Mahusiano wa benki
hiyo, baada ya makabidhiano hayo.
Picha na Muhidin Sufiani-OMR