JOSHUA NASSARI AENDA KUTOA DAMU KWA AJILI YA WAATHIRIKA WA MLIPUKO ULIOTOKEA KANISANI ARUSHA

Joseph Pantaleo, Arusha Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari Akitoa Damu kwa ajili ya kuwasaidia majeruhi wa mlipuko wa bomu Leo jijini Arusha.
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari mbali ya kuwahamasisha watu kutoa damu, pia hivi punde amemaliza kutoa damu kwa ajili ya kuwachangia majeruhi waliolipukiwa na bomu kanisani LEO. Pichani Nassari akionekana akitoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari LEO tangu majira ya saa 5:30 asubuhi wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahamasisha watu kutoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi mbalimbali waliojeruhiwa na bomu katika kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti mjini humo.

Kutokana watu wengi kupoteza damu na kumwagika kwa wingi. Mbali na hilo baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo wamesema kwamba hivi sasa wana wakati mgumu katika kufanya usafi na mwandishi wetu Joseph Pantaleo ameshuhudia manesi hao wakisafisha damu sakafuni kila wakati huku wakimwaga maji na dawa ili kuondoa mabaki ya damu hiyo.

Lema na Nassari wameonekana wakiwahamisisha watu kutoa damu na wengi wameitikia wito huo. Endelea kusoma habarimasai.com kwa taarifa mbalimbali zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo