Makete
Wilaya ya Makete mkoani Njombe imejipanga kuhakikisha
inawachukulia hatua za kisheria wazazi wa wanafunzi ambao hawajaripoti shuleni
hasa wa kidato cha kwanza, kutokana na wazazi wengi kuwa ndiyo sababu
inayopelekea wanafunzi hao kutofika shuleni
Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Makete mh Josephine
Matiro wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za serikali kwa
kipindi cha Januari-Aprili 2013 katika wilaya yake
Matiro amesema amegundua wapo baadhi ya wazazi wa Makete
ambao huwatorosha watoto wao na kwenda kuwapeleka kufanya kazi hasa za ndani
nje ya wilaya yake ilihali watoto hao walifaulu kwenda kidato cha kwanza
“Wazazi mnatakiwa kufahamu urithi wa mtoto ni elimu na
inasikitisha sana kama humpeleki mtoto wako shule ili akawe housegirl au
houseboy mijini, naimani watoto hao lazima waje kuwalaumu nyie wazazi kwa
kutompa elimu” alisema Matiro
Amesema kwa hivi sasa tayari wameanza kuushirikisha uongozi
wa kata na vijiji kuwasaka wazazi na walezi wa watoto ambao hawajaripoti
shuleni ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria
Jumla ya wanafunzi 2,173 waliochaguliwa kujiunga na kidato
cha kwanza wilaya ya Makete mwaka huu 532 hawajajiunga na masomo hayo hadi sasa
Taarifa hiyo ya mkuu wa wilaya iligusa Nyanja mbalimbali
ikiwemo, Elimu, afya, maji, kilimo, barabara, maliasili na utalii
Na Edwin Moshi, Makete