TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MBEYA

MNAMO TAREHE 23.04.2013 MAJIRA YA SAA 10:00HRS HUKO KATIKA KIJIJI CHA
 MAWELO WILAYA YA CHUNYA MKOA WA MBEYA. LAISON S/O MJAHA, MIAKA 78, MKULIMA,KYUSA, MKAZI WA KIJIJI CHA MAWELO.

ALIKUTWA NYUMBANI KWAKE  AKIWA AMEUAWA KWA KUPIGWA SULULU KWENYE PAJI LA USO NA MTU/WATU WASIOFAHAMIKA.

  CHANZO NI IMANI ZA KISHIRIKINA KWANI MAREHEMU ALIKUWA ANATUHUMIWA KWA MUDA MREFU KUWA NI MCHAWI HAPO KIJIJINI.MBINU ILIYOTUMIKA NI KUMVAMIA AKIWA AMELALA NDANI YA NYUMBA YAKE NA KUMUUA.

 KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
BARAKAE MASAKI  ANAENDELEA KUTOA WITO KWA JAMII KUACHANA NA IMANI POTOFU ZA KISHIRIKINA KWANI ZINA ATHARI KUBWA KWA JAMII NA KURUDISHA NYUMA MAENDELEO.
 
Signed By,
 [BARAKAEL MASAKI  – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo