MWANAMKE AVUA NGUO ASIKAMATWE NA DAWASCO



Picha  hii  si  ya  tukio hilo...

OPERESHENI ya kuwasaka wezi wa maji Dar es Salaam, juzi imechukua sura mpya baada ya mkazi wa Tandale Chama, wilayani Kinondoni ambaye ni mwanamke , kuvua nguo zote.

Chanzo cha mwanamke huyo kuvua nguo ni baada ya kuuona msafara wa Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Meck Sadiki na Maofisa
wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka (DAWASCO), ambao walimkuta akiuza maji aliyojiunganishia kiholela.
 
Hata hivyo, Ofisa wa DAWASCO ambaye ni mwanamke alilazimika kumkamata na kuwekwa chini ya ulinzi wa polisi waliokuwa katika operesheni hiyo.
Operesheni hiyo ilifanyika kwenye eneo la Kagera, Tandale Chama, Mkwajuni na Bonde la Mkwajuni ambapo vifaa mbalimbali ambavyo vilikuwa vikitumika kuunganisha maji vilikamatwa.
 
Mkuu wa Mkoa huo, Bw. Sadiki alisema operesheni hiyo imefichua mambo mengi yanayofanywa na wananchi aliowaita wahujumu uchumi kwa kujiunganishia maji kiholela bila kuyalipia.
 
Alisema asilimia 36 ya maji yamekuwa yakipotea kutokana na baadhi ya watu kujiunganishia kichume cha sheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo