DAR ES SALAAM, Tanzania
Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahiman Kinana anawatakia
Wakristo na watanzania wote kwa ujumla sikukuu njema ya Pasaka.
Ndugu Kinana amesema "Ni vema watanzania kwa pamoja kusherehekea sikukuu hii ya Pasaka kwa unyenyekevu na utulivu.
Ndugu
Kinana amewaasa pia Watanzania kuitumia sikukuu hii kutafakari kwa kina
na kumwomba Mungu aendelee kuijalia nchi yetu ya Tanzania ili iendelee
kuwa kisiwa cha amani na utulivu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na
kijacho.
CCM
inaamini kuwa wajibu wa kuilinda Amani, upendo na umoja ni ya kila
mwananchi na kwamba la msingi ni kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake.