Wakazi
wa madizini kata ya boma mkoa wa Morogoro wameandamana kupinga miti
iliyo katika mtaa wao kukatwa kwa kuwa hawakushirikishwa na viongozi wa
mtaa wao
wakazi hao wengi wakiwa vijana walindaman leo asubuhi kwa
kuzunguka maeneo yote ambayo miti tayari imeshakatwa kwa lengo la
kusimamisha zoezi hilo kwa kuwa halikufuata utaratibu.
Wakazi hao pia wamelalamikia vibali vivivyotumika kutokuwa halali,Vijana hao wakizungumza asubuhi ya leo wamemuomba mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera kuingilia Mgogoro huo kwa lengo la kunusuru maliasili hiyo ambayo inatoweka kwa kasi mtaa wa madizini kata ya boma mkoani morogoro.
Wakazio hao wanapingana na viongozi wao akiwepo diwani ya kata hiyo Mh Amir Nondo na mwenyekiti wa mtaa aliyefahamika kwa jina moja la Mashaka.
Waandishi wa habari wakiwa eneo hilo kujua mengi zaidi kutoka mtaa huo kuhusu mgogoro huo
Miti iliyovunwa ambayo inalalamikiwa na wakazi wa mtaa madizini kata ya boma mkoani Morogoro.picha zote na morotownrecords blog