TIMBULO ANENA KUHUSU TUHUMA ZA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA


Tangu jana  kumekua na story zilizoenea mitaani kuhusu Mwanamuziki Timbulo kukamatwa na madawa ya kulevya Nchini Burundi. Picha  zake zilizagaa katika  mtandao wa facebook  zikimuonyesha timbulo akiwa chini ya ulinzi wa police na kidhibiti chake cha madawa haya ambayo yamefungwa kwa mfano wa pipi...

Ilinibidi nimtafute timbulo kupitia mtandao wa whatsup ambapo nilimuona akiwa active kama dakika kumi zilizopita mara baada ya kupata habari hizo

Timbulo amesema ni kweli alihisiwa kuwa amebeba madawa ya kulevya kitu kilichowafanya wanausalama kuomba kumkagua na kweli kumkuta na Pipi ambazo mara nyingi zimekua ni mfumo wa kubebea madawa ya kulevya katika begi lake, lakini katika maelezo ya timbulo anasema hazikuwa dawa za kulevya kweli bali ni mfano wa dawa ambazo alifanyia shooting katika movie yake ya hivi karibuni na kusahau kuzitoa. 


Hata hivo kutokana na maelezo yake anasema alihisiwa zaidi kubeba mzigo huo kutokana na mtu aliekuja kumpokea kusadikika kuwa katika biashara hiyo.

Timbulo alikua nchini burundi kwa shughuli zake za kimuziki akiwa ametokea Bukoba alikokua na shows huko lakini pia ikiwa ni mwendelezo wa safari ya kumfikisha Younde Cammeron ambako pia alikua anaenda kwa shughuli zake za kimuziki. Safari zote hizo ziliishia hapo baada ya tukuo hilo na hivi mpaka naingia mtamboni timbulo aliniambia yupo jijini mwanza kwa safari ya kurudi Dar Es Salaam.
CREDITS:MPEKUZI 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo