Hili ndilo gari la Hayati Mwalimu Nyerere na kwa mara ya mwisho alilipanda 31/08/1999 kutoka nyumbani kwake Msasani jijini Dar es Salaam hadi Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupanda ndge kwenda London Uingereza kwa ajili ya matibabu, lakini Mwalimu hakurejea tena Tanzania akiwa hai, na alifariki 14.10.1999 katika hospitali ya mtakatifu thomas huko Uingereza
Mjane mama Maria Nyerere alilitoa rasmi gari hili kwa serikali 24.09.2004 ili liwekwe kwenye makumbusho ya taifa kama kumbukumbu nzuri kwa Taifa hili