SERIKALI WILAYANI MAKETE KUKABWA KOO NA CCM


Chama cha mapinduzi(CCM) wilayani Makete kimedhamiria kuendelea kuibana serikali wilayani humo kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wananchi wake kama ilivyo adhma ya serikali ya kutoa huduma bora kwa wananchi wake

Akizungumza na mtandao huu ofisini kwake katibu wa CCM wilaya ya Makete Miraji Mtaturu amesema kwamba kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa ilani ya chama chake kwa kipindi cha mwaka mmoja 2011/2012 iliyosomwa na serikali katika kikao cha halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Makete, wao kama chama wamegundua kuwa bado kuna kusuasua katika utekelezaji wa miradi ya kilimo, afya, miundombinu na utawala bora

Amesema ingawa kuna uhaba wa wagani kazi katika sekta ya kilimo lakini hao waliopo baadhi yao hawatendi kazi zao ipasavyo hali ambayo inapelekea usumbufu kwa wananchi hususan wakati wa kupatiwa pembejeo za kilimo

“Kwa mfano pale kwenye kata ya Isapulano tumeelezwa wakala ameleta mbolea muda mrefu lakini bado hajaisambaza kwa wananchi, sisi tumeagiza kupitia kikao kile kuwa halmashauri kupitia idara ya kilimo ilifuatilie hilo mapema kabla msimu haujapita, na pia afisa kilimo wa kata hiyo anaonesha uzembe mahali Fulani” alisema Mtaturu

Kata hiyo ambayo pia inachangamoto ya barabara kutopitika Mtaturu amesema kikao hicho kimemuagiza mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Makete, kuhakikisha barabara hiyo inapitika na kuwatolea adha wananchi ambao huitumia kusafiri kwenda mkoani Mbeya

“mkurugenzi alitueleza kuwa fedha ya matengenezo ya barabara hiyo ipo na mkandarasi ameshapatikana lakini kinachosubiriwa ni msimu wa mvua upite ndipo matengenezo yafanyike lakini sisi kama chama tumemtaka mkurugenzi na mhandisi wa ujenzi wilaya kufanya maarifa na matengenezo madogomadogo ya mashimo hayo ili barabara hiyo ipitike wakati huu wa masika ili iwasaidie wananchi” alisema

Kuhusu suala la afya kikao hicho kimeiagiza serikali kuhakikisha inaendelea kutoa elimu ya watu kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) ambapo bado kuna maeneo mengine wananchi wamekuwa wagumu kuchangia kumbe hali hiyo inasababishwa na wao kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu elimu hiyo

Mtaturu amesema pia suala la matibabu bure kwa wazee nalo litiliwe mkazo kwani kumezkuwa na malalamiko kutoka kwa wazee wengi kuwa bado wanatozwa fedha pindi wanapokwenda kupatiwa matibabu ilihali wana miaka 60 na kuendelea


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo