Gari la
Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA likirejea katika Ofisi ya Kanda ya
Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la SELOU likitokea ndani ya Pori
Hawa ni wafanyakazi wa Game frontiers of Tanzania wakiwa wamebeba pembe za ndovu
Pembe za ndovu, Risasi na Silaha zilizokamatwa
………………………………………………………………………………..
Na Hamza Mashole wa Songea- ( www.demashonews.blogspot.com)
Kampuni ya
GAME FRONTIERS OF TANZANIA kwa kushirikiana askari wanyamapori wa Selou
na Askari wa vijiji vinavyozunguka pori la Akiba la Selou wamefanikiwa
kukamata meno ya tembo 15 yenye thamani ya milion miambili, Risasi 9,
Bunduki moja aina ya RIFFLE 458 na Gobole moja ambavyo hutumika kuulia
wanyama.
Doria hiyo
imechukua takribani siku tatu katika pori la Akiba la Selou ikiwa ni
sehemu ya kuwatafuta majangili wanaofanya mauaji ya wanyamapori katika
pori hilo,
Akizungumza
na mwandishi wetu Bw. Mohamed Mpapa ambaye ni mwakilishi wa kampuni
hiyo ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA, Amesema kuwa hiyo ni kujituma
kutokana na motisha ya fedha anayoitoa mwezeshaji wa kampuni ya GAME
FRONTIERS OF TANZANIA ndio chachu ya mafanikio ya kukamata meno,bunduki
na risasi.
Akiendelea
kuzungumzia tukio hilo Bw. Mohamed Mpapa amesema baada ya majangili
kuwaona Game Frontiers Tanzania wakiwa katika doria ndani ya pori hilo
huku wakiwa wamekamilika kimapigano majangili hao waliweza kukimbia na
kuacha nyara hizo baada ya kuona nguvu yao ni ndogo katika kupambana na
kundi la doria.
Ameongezea
kwa kusema Kampuni yake imefurahishwa na mafanikio na ushirikiano
uliopo kati yao, Serikali na wanavijiji kukabiliana na ujangili
unaoendelea kuwamaliza tembo katika Pori la Akiba la Selou pia ametoa
wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano katika kuwafichua majangili.
Nae Kaimu
Mkuu wa Kanda ya Kusini Magharibi ya Pori la Akiba la Selou Bw. Bernald
Lijaji amesema Pembe zilizokamatwa ni 15 pamoja na Bunduki aina ya RIFLE
458,Gobole moja na Risasi 9 aina ya 458 vimekamatwa katika Doria
iliyofadhiriwa na Mwekezaji wa Kampuni ya GAME FRONTIERS OF TANZANIA