LULU ambaye kwa sasa yupo uraiani kwa dhamana
huku kesi yake ya tuhuma za kuua bila kukusudia ikiendelea, amesema kuwa
hajafungua taasisi yoyote wala kuomba misaada kupitia mtandao wa
kijamii wa Facebook.
Nasikia tu kwa watu eti sijui ninataka wasanii waigizaji kwa ajili
ya taasisi yangu, mara nimetoa namba ya simu watu wanichangie ili
nitengeneze filamu, sijafanya kitu kama hicho na wala siwezi nahitaji
kutulia na kuangalia mambo yangu, alisema.
Hivi karibuni kupitia facebook kumeonekana akaunti inayotumia picha na majina ya Lulu kwa kuwaomba wadau wa filamu wamchangie fedha kwa njia ya m-pesa na tigo-pesa.
Lulu anatuhumiwa kuhusika na kifo cha aliyekuwa msanii wa filamu, Steven Kanumba, kilichotokea mwaka jana.
SOURCE:MWANASPOTI