
katibu
mkuu
wa chama cha CCM, Abdurahman Kinanan akifungua pazia kuzindua tawi
jipya la chama hicho ndani ya kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani
Kigoma mapema leo jioni.

Jiwe la Msingi lililowekwa na Ndugu Kinana.


Ndugu kinana akishiriki ujenzi wa ofisi ya tawi jipya la chama cha CCM kata ya Bunyambo,Wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma mapema leo jioni.

Ndugu Kinana akisomewa taarifa kutoka kwa wanachama wa chama cha CCM,mapema leo jioni.

Ndugu
Kinana akizungumza na wanachama wa chama hicho sambamba na wananchi wa
kata hiyo ya Bunyambo,Ndugu Kinana aliahidi kutoa kiasi cha shilingi
milioni mbili kukamilisha ujenzi wa tawi hilo jipa la chama hicho.

Ndugu
Kinana akizungumza na Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya
Kumwambu,Wilaya ya Kibondo,Ndugu Kinana alikwenda shuleni hapo kukagua
maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo na pia kushiriki ujenzi wake,pia
aliahidi kutoa Solar Pannel kwa ajili ya kuzalisha umeme ofisi za
walimu,Kompyuta moja,seti ya jezi mbili sambamba na mipira miwili kwa
ajili ya shule hiyo.

Ndugu
Kinana akishiriki ujenzi wa shule ya sekondari ya Kumwambu akiwa
sambamba na baadhi wa viongozi wa Wilaya na mkoa kutoka chama cha CCM.

Wazee
wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani Wilaya,Wazee pamoja na Jumuiya
kwa ujumla wakishangilia jambo kwenye mkutano wao wa ndani uliofanyika
kwenye ukumbi wa Vijana,wilayani Kibondo.

Ndugu
Kinana akizungumza na Wazee wa chama wa shina,Matawi,kata,Madiwani
Wilaya pamoja na Wazee,lengo ikiwa ni kuwasilisha taarifa ya kazi za
chama na serikali,Ndugu Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi milioni
kumi kwa ajili ya kusaidia shunguli mbalimbali za Vijana sambamba na
hilo Kinana ameahidi kutoa kiasi cha shilingi Milioni tatu kwa ajili ya
kuwasaidia Walemavu.Mkutano huo umefanyika leo kwenye ukumbi wa
Vijana,wilayani Kibondo,Mkoani Kigoma.

Ndugu
Kinana akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kibondo,Emmanuel
Gwegenyeza,pichani kati ni Mkuu wa Wilaya ya Kibondo,Venance Mwamoto
pamoja na Kada wa chama hicho,Matoni Nyobeye,mara baada ya kuwasili
kijiji cha Kilemba,wilayani Kibondo mapema leo jioni.
Msafara wa Ndugu Kinana pamoja na baadhi ya viongozi wa juu wa chama cha CCM,Mkoa na Wilaya