Jaji Lisa Traylor-Wolff |
Jaji wa Indiana mwenye miaka 52
anakabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya taaluma yake baada ya kudaiwa
kufanya mapenzi na mfungwa ambaye ana umri nusu yake katika chumba cha
mahojiano wakati mfungwa huyo akiwa bado kifungoni.
Lisa Traylor-Wolff anafanya kazi ya muda maalumu kama Jaji wa daraja la juu katika mahakama mbili za kaskazini kwa Indiana. Pia anafanya kazi kama wakili wa utetezi.
Tume ya Sifa za Idara ya Mahakama imesema alianza 'mahusiano ya kimwili na mteja wake mfungwa huyo mwenye miaka 26' ambaye alikuwa akimwakilisha katika kesi binafsi.
Mahusiano hayo yalidaiwa kuendelea baada ya kuwa amehukumiwa kifungo gerezani. Lisa alimwakilisha mfungwa huyo wakati alipokata rufani kupinga hukumu hiyo, kwa mujibu wa gazeti la Indianapolis Star.
Tume hiyo ilibaini kwamba alikuwa na 'mahusiano yasiyokubalika' na kijana huyo ndani ya chumba cha kukutania mwanasheria na mteja katika Jengo la Marekebisho la Miami huko Peru, Indiana.
Lisa hakuomba mkataba mpya wa ujaji wake kwa mwaka 2013.
Ana siku 20 kujibu tuhuma hizo na baada ya hapo, kesi hiyo itafikishwa kwenye Mahakama Kuu ya Indiana.
Hapo kabla alifanya kazi kama Jaji wa Mahakama ya Juu katika Mahakama ya Pulaski na alikuwa mkuu wa Chama cha Majaji katika mahakama yake.
Lisa hakujibu chochote kuhusu madai hayo.
Awali alituhumiwa kuvunja sheria nne zinazohusu taaluma yake, ikiwamo miiko inayokata mwanasheria kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mteja wake, kuzuia mwanasheria kumwakilisha mteja endapo kuna ushahidi dhahiri kwamba uwakilishi huo unasukumwa na utashi binafsi wa mwanasheria.
Pia anatuhumiwa kwa kudharau uhuru wa uaminifu na uadilifu kama jaji.
Endapo Lisa atapatikana na hatia, Mahakama Kuu ya jimbo hilo inaweza kumfungia kuendesha ofisi ya mashitaka katika jimbo hilo - kwa muda hadi kufikia kifungo cha maisha.
Haijafahamika endapo Chama cha Majaji cha Indiana pia kinachunguza kesi hiyo.
Lisa ambaye alihitimu katika Chuo Kikuu cha Sheria cha Valparaiso mwaka 1986 - mwaka ambao anayedaiwa kuwa mpenzi wake huyo alizaliwa.