MSANII wa filamu ambaye amekuwa kimya kwa muda mrefu, Aisha Bui amesema kuwa kwa sasa anasubiria muda wa kufanyiwa upasuaji wa matiti yake kabla ya kurejea kwenye fani.
Aisha Bui.
Akizungumza hivi karibuni, Aisha alisema kuwa zoezi la
upasuaji huo litafanyika Machi mwaka huu huko Afrika Kusini lengo
likiwa ni kutengeneza muonekano anaoutaka.
“Nimekuwa na muonekano nisioupenda, sipendi haya matiti makubwa ndiyo maana nimeamua kufanya upasuaji, nimeambiwa inawezekana na nitafanya hivyo mwezi wa tatu,” alisema Aisha na kuongeza:
“Najua wapo wanaojiuliza niko wapi, nimejichimbia huku Sauzi na nikirejea sanaa kama kawa.”
NA GPL