Wakiwa katika picha ya pamoja watoto
ambao ni mapacha watatu, Rehema, Amani na Neema.
Na Kalisa Kachuchu wa Kajunason
Blog, Dar es Salaam.
Mkazi wa Kimara, jijini Dar es
Salaam, Edwin Rweyongeza, amewaomba Watanzania kumsaidia kuwatunza
watoto wake mapacha watatu ili waweze kukua vizuri kutokana na matatizo
ya kipato yanayomkabili.
Rweyongeza, aliitaja misaada hiyo
kuwa ni pamoja na Chakula cha watoto lishe, yakiwamo maziwa pamoja na
matibabu ya kuishiwa na damu yanayoendelea kuwa tatizo kwa watoto wake.
Akizungumza muda mfupi uliopita na
Habari na Matukio Blog, Rweyongeza alisema ukosefu wa kipato
unaomsumbua, unamfanya ashindwe kuwamudu watoto hao waliozaliwa Julai
sita mwaka 2011 katika Hospitali ya Mwananyamala.
Alisema kutokana na ukosefu wake wa
kipato, Ustawi wa Jamii wilaya ya Kinondoni, ilikubali Rweyongeza apate
msaada kutoka kwa jamii, kwa barua yao waliyoandikaa Septemba 14, mwaka
2011 yenye kumbukumbu namba W/WG/2011 na kusainiwa na A.Mbusa.
“Naomba msaada kutoka kwa Watanzania
wenzangu na Dunia kwa ujumla ili watoto wangu waweze kupata lishe na
kufanikisha maisha yao, maana mimi baba yao kwa sasa sina kipato
chochote kwasababu sina kazi ya kuniingizia kipato.
“Kama ningekuwa na uwezo nisingeomba
msaada, ukizingatia kwamba watoto watatu kuwalea ni kazi kubwa, hasa kwa
masuala ya lishe na matibabu, kama vile maziwa na mengineyo
yanayochangia kukua vizuri,” alisema Rweyongeza.
Kwa wenye moyo nahitaji la kumsadia,
kijana huyo mwenye miaka 29, alizitaja namba zake ni 0767 646599, 0719
909085, huku akitanguliza shukrani zake za dhati kwa Watanzania wote.
Mkazi wa Kimara, jijini Dar
es Salaam, Edwin Rweyongeza akiwa na familia yake kwa ujumla.
