Head of Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia)
ambaye pia ni mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa
Afya ya Mama na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni
kuongeza kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na
Watoto na kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na
Mtoto. Kutoka kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital
Dr. Ambrose Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin
Habib, Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian
Ndege na Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo
Bw. Anis Nazrani.
Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege
(wa pili kushoto) akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba
wagonjwa kwa hospitali ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa
vinavyotokea katika hospitali nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na
watoto wasio na hatia ambao hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo
usafiri na hivyo katika kujali hilo wametoa magari hayo.
Aidha
amesema Ndege Medics inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa
kujaribu kuokoa maisha ya akina mama na watoto ambao lengo lake ni
kuchangia katika kuboresha afya ya uzazi wa mama na watoto wachanga
katika mikoa ya Dodoma, Iringa, Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr.
Sebastian Ndege wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba
wagonjwa kwa Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha
Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania
Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
Pichani Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa
kwa ndani yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa
ajili ya mradi wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Pichani
Juu na chini ni baadhi ya Wafanyakazi wa Kampuni ya Ndege Medics,
Hospitali ya Aga Khan na waandishi wa habari walioshuhudia tukio la
makabidhiano hayo.
Baadhi
ya magari ya kubebea wagonjwa yaliyokabidhiwa rasmi leo kwa Hospitali
ya Aga Khan jijini Dar ikiwa ni sehemu ya mradi Endelevu utakaohusisha
Mikoa ya Mwanza, Dodoma, Iringa, Mbeya na Morogoro kwa ajili ya
kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto.