MWENDESHA PIKIPIKI AFA BAADA YA KUGONGWA NA DALA DALA JIJINI MWANZA

Askari wa usalama barabarani wakipima ajali iliyotokea leo jioni eneo la Igoma jijini Mwanza na kusababisha kifo cha mtu mmoja ambaye anatajwa kuwa ni abiria ambaye alikuwa amembeba dereva wa pikipiki iliyopata ajali yenye namba za usajili T988 BDW ambapo dereva wake (ambaye ndiye mmiliki aliyekuwa amepakizwa) alikimbia mara baada ya ajali hiyo kutokea, inasemekana kuwa pikipiki hiyo iliyokuwa kwenye mwendo kasi iligonga kwa nyuma basi la abiria aina ya daladala lenye namba za usajili T768ASA lililosimama ghafla mbele ya pikipiki hiyo kwa ajili ya kupakia abiria.
Kijana aliyefariki  alitambulika kwa jina la Mayunga Clement Lufuta.

Pikipiki hiyo yenye namba za usajili T988 BDW eneo lake la mbele limezama kabisa uvunguni mwa daladala kiasi cha kuharibika vibaya.

Pikipiki iliyopata ajali ikiondoshwa barabarani kwa amri ya trafiki.
Kisha mwili wa marehemu Mayunga Clement Lufuta ukatolewa barabarani kusubiri gari maalum kupelekwa hospitali ya rufaa Bugando kuhifadhiwa.
Hiki ndicho kitambulisho kilichosaidia kumtambua marehemu. Picha zaidi gsengo.blogspot.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo