DAR ES
SALAAM, Tanzania
MAALIM Hassan
Yahya Hussein, amepinga kauli
iliyotolewa hivi karibuni na mtabiri mwenzake kuwa rais wa mwaka 2015
kuwa
atakuwa mwanamke.
Akizungumza na
wandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu utabiri wake wa
matukio yatakayotokea mwaka 2013, ambapo mwaka huo utaanza Machi 21
mwaka huu.
Maalim Hussein
alisema kiutabiri huwezi kutoa utabiri
katika matukio ya mwaka mmoja mbele, kitendo cha mtabiri huyo ni sawa na
kuwakatisha tamaa baadhi ya watu wenye nia ya kutaka kugombea nafasi
hiyo mwaka
2015.
“Huwezi kutoa
utabiri wa miaka miwili mbele hata
Sheikh Yahya Hussein mtabiri aliyekuwa akikubalika hakuwahi kufanya
hivyo, pia
sikubaliani naye kuwa rais ajaye atakuwa mwanamke hata ukiangalia katika
njia
zetu za utabiri ambazo ni namba zinapingana na hilo”alisema.
Alisema matokeo
ya utabiri kama huo ni sawa na
uwamuzi wa kuwafungia milango kidemokrasia baadhi ya wanasiasa wenye nia
ya
kugombea urais mwaka 2015.
“Kuna baadhi ya
viongozi wakiwemo Lowassa na Membe
wanadaiwa kuwa huenda wakagombea nafasi hiyo, kwa kufanya hivyo itakuwa
ni
kuwakatisha tamaa”alisema.
Akizungumzia
utabiri wa mwaka huu, alisema kuwa kuna
viongozi wengi, wabunge, wakuu wa mikoa na wengine watatoa matamshi ya
utatanishi na kusababisha hofu na mitafaruku
itakayowafanya watu kupigana.
Vile vile
alisema wapo wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
wataungana
katika masuala ya msingi yatakayohusu utaifa bila kujali itikadi zao za
kivyama
au kimajimbo.
Maalim Hussein
alibainisha kuwa Rais Jakaya Kikwete
ataunganisha nchi na kuwa moja yenye uimara wa utaifa kuliko watangulizi
wake,
akishirikiana zaidi na wanasiasa na viongozi wa dini kuondoa mtikisiko
wa
uvunjifu wa amani uliyojitokea mwaka jana.
Aidha, Chama
kimoja cha siasa kitajitokeza na
kitachochea kujitenga na kuunda Taifa lake hata hivyo, kusudio hilo
halitafanikiwa kwani litapingwa na Watanzania wote kwa kauli moja na
vitendo.
Maalim Hussein
pia alisema kutatokea vifo vya ghafla
kwa watunzi wa hadithi na vitabu, wandishi wa habari, wanasiasa na
wasanii
ambapo matukio hayo yatakuwa mabaya zaidi kuliko mwaka jana.
Akigusia
Uchaguzi Mkuu utakaofanyika hivi
karibuni nchini Kenya ambao ni
majirani, alisema kuwa Muungano wa CORD, ukiongozwa na Raila Odinga
utashinda
uchaguzi huo, ambao ana amini utakuwa wa amani na tulivu.
“Ushindi huo
utakuja baada ya kuushinda Muungano wa
Jubilee ukiongozwa na akina Uhuru Kenyata na Ruto pamoja na ule wa
Musalia
Mudavadi unaoitwa AMANI”alisema.