![]() |
| Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Tarime na Rorya Justus Kamugisha |
JESHI la
Polisi katika
Kanda Maalumu ya Tarime na Rorya, linamshikilia Prisca Mwita mwenye umri
wa
miaka 22, mkazi wa Mtaa wa Nyamisangura, mjini Tarime, kwa tuhuma za
kumuua
mtoto wake mchanga na kumnyofoa baadhi ya viungo vyake.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya
Tarime na
Rorya, Justus Kamugisha, amesema kuwa, tukio hilo limetokea Januari 11,
mwaka
huu, majira ya saa 2:00 asubuhi nyumbani kwa mwanamke huyo.
Amesema kuwa,
mwanamke
huyo, anatuhumiwa kumuua mtoto wake, Happy Anthony, mwenye umri wa miezi
11,
baada ya kumkata sikio la kushoto, kumnyoa nywele za upande wa kushoto,
kumnyoa
nyusi za jicho la kushoto na kumchuna ngozi ya kichwa sehemu ya kushoto.
Ameongeza
kuwa, majirani
wamegundua unyama huo na kutoa taarifa kwa viongozi wa eneo hilo,
kitendo
ambacho kimesaidia kutiwa mbaroni kwa mtuhumiwa.
Kufuatia
tukio hilo,
wananchi wa eneo hilo wamehusisha tukio hilo na imani za kishirikina,
kwani ni
la ajabu kwa mama mzazi kufanya unyama dhidi ya mtoto wake.
