Bango
la mahakama ya hakimu mkazi mjini Singida.(Picha na Nathaniel Limu).
Na
Nathaniel Limu.
Jumla
ya raia 12 wa nchini Ethiopia wamehukumiwa na mahakama ya wilaya ya
Singida kulipa faini ya shilingi laki moja (100,000) kila mmoja, baada
ya kukiri makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania bila ya kuwa na kibali halali.
Pia
mahakama hiyo, imeamuru basi la kampuni ya Mtei ya mjini Arusha T.797
CDZ lililokuwa limewabeba Waethiopia hao, likamatwe na kutaifishwa kuwa
mali ya serikali.
Waethiopia
hao wote bado ni vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa shule na
vyuo.
Baada
ya nwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Ahmed Seif kuwasomea
makosa hayo mawili ya kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na kibali,
washitakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa
hayo.
Kabla
ya kutolewa kwa adhabu hiyo, mwanasheria wa serikali Seif aliiomba
mahakama hiyo kuwa iwape adhabu kali washitakiwa ikiwa ni njia moja wapo
ya kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila
ya kuwa na kibali cho chote halali.
Akitoa
hukumu hiyo hakimu mfawidhi kiongozi wa mahakama ya wilaya ya Singida
Flora Ndale, amesema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na
upande wa mashitaka na utetezi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya
kulipa faini ya shilingi laki moja kwa kila mshitakiwa.
Hata
hivyo, washitakiwa wote 12 kila mmoja wao alilipa faini hiyo ya
shilingi laki moja na hivyo kuachiwa huru.
Kwa
mujibu wa mwanasheria wa serikali Seif, washitakiwa hao walikamatwa
Januari 17 mwaka huu alasiri katika eneo la kijiji cha Kititimo nje
kidogo ya mji wa Singida, wakiwa wametokea mkoani Arusha wakielekea
nchini Afrika kusini.