
KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana
---
KATIBU Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana amekerwa na chokochoko za
kidini zilizoanza kujipenyeza hivi karibuhi na kutoa wito kwa madhehebu
ya dini na taasisi zake hapa nchini,kuendelea kuhubiri amani kwa
kuliombea taifa,ili wananchi waendelee kujivunia amani iliyoachwa na
Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.
Kinana alitoa kauli hiyo juzi kwenye maadhimisho
ya siku ya kumbukumbu ya Imam Husein, yanayoadhimishwa na dhehebu la
KhojaShia Ithna Asheri Jamaat Arusha kote duniani na kufanyika kwenye
msikiti wa jumuiya hiyo jijini hapa,ambapo watu mbalimbali wakiwamo
viongozi wa madhehemu pamoja na viongozi wa chama na Serikali
walihudhuria.
Kinana alisema kuwa upo umuhimu mkubwa kwa
viongozi wa dini na taasisi zake kuendelea kuienzi amani kwa kuhubiri
suala la kudumisha amani na kuonya kwamba Serikali haitasita kuchukua
hatua za haraka kwa mtu ama kikundi chochote cha dini kitakachojihusisha
na uvunjivu wa amani.Kwa habari zaidi Bofya na Endelea......>>>>>